Katika tathmini nilioifanya mimi binafsi ni kwamba Bei za vitu mbalimbali katika mkoa wa iringa inashahabiana sawasawa na bei za vitu katika mkoa wa Arusha. Kwa tathmini hii inaonyesha dhahiri kua mkoa wa iringa ni mkoa unao kua kwa kasi zaidi.
Kiwanja cha mpira chenye nyasi bandia iringa |
Ukiachana na vitu pia bei ya kiwanja au ardhi ni gharama sana kulingana na uchumi wa raia mwenye kipato cha chini. Licha ya hayo mkoa wa iringa sasa ni mkoa wenye vituo vya radio si chini ya Tisa, vyuo vikuu na vyuo vya ufundi vinaendelea kuongezeka katika mkoa huu.
Iringa ni mkoa ambao una ongezeko la magari na kuwa na foleni zadi hasa saa za asubuhi. Viwanda vingi vilivyopo Iringa, viwanja vya michezo, barabara za kisasa na vyuo ni moja ya vitu vilivyo fanya iringa kua na watu wengi na kuongezeka kila kukicha. Hii ndio irnga yetu.