WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Monday, September 16, 2013

JE WAJUA MADHARA YA MITANDAO YA KIJAMII?

                     
Kiukweli kabisa pasipo kumeng'enya maneno, nchi zinazoendelea hususani nchi yetu ya Tanzania, muingiliano wa mitandao ya kijamii imeleta changamoto nyingi sana.

                           
Waangalie vijana wetu wenye miaka kuanzia 15-24 uone namna gani wameathirika na matumizi ya mitandao ya kijamii. Lakini pia waangalie baadhi ya vijana hasa wa kiume walivyokosa ustaarabu kwa kutumia mitandao ya kijamii kutongoza watoto wa kike! Sikatai, mnapokutana ndo mwanzo wa mambo mengine, lakini inapofikia wakati mtu kazi yake leo anamtongoza huyu, kesho karukia kwa yule tayari hapo tunakuhesabu wewe ni limbukeni wa maisha ya mtandaoni na maisha ya kawaida. Ifike wakati vijana hawa watambue kuwa mitandao ya kijamii ina staha yake.
                             
Watu wanasadiki kwamba pamoja na kuwasaidia watu kuwasiliana kwenye mitandao ya kijamii lakini pia inawapa watu nafasi ya kuwa na uzoefu katika matumizi ya kompyuta, simu, tablets n.k. Lakini pia watu wanasadiki pia matumizi ya mitandao ya kijamii inawafanya watoto kuwaweka mikononi mwa manyang'au pasipo kupenda, unaongeza nafasi ya kompyuta kushambuliwa kirahisi na virusi, lakini pia inapunguza sana utendaji wa kazi maofisini. Fikiria jinsi siku hizi wafanyakazi maofisini ni kwa kiwango gani wanatumia muda wao kwenye mitandao ya kijamii. Mtu yuko radhi aache kufanya kazi za ofisi zinazomlipa mshahara na kumfanya aishi mjini, anaendelea kuchati kwenye mitandao ya kijamii. Hii ndiyo teknolojia yetu. 
                                                    
Mwaka 2009 kwenye uchaguzi wa Iran, kulikuwa na uasi mkubwa katika nchi hii ambao nyuma ya pazia nchi ya marekani kwa ushirikiano mzuri sana na twitter waliendesha zoezi la uasi huu. Mapinduzi mbali mbali ambayo yametokea kwenye nchi mbali mbali miaka ya hivi karibuni imechangiwa sana na mitandao ya kijamii.
                         
Uchaguzi wa urais nchini marekani mwaka 2008 jamii ya kimarekani ilikuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kiwango kikubwa na hivyo kusaidia kufanya kampeni za uchaguzi kwa kasi kubwa sana. Kwa mfano, mgombea (wakati huo) Baraka Obama alikuwa na wafuasi kwenye facebook 2,379,102. Takwimu za Juni, 2012 inaonyesha Obama ana mashabiki 27,107,496 duniani kote kwenye mtandao wa facebook tu.
                         
Inasadikika kuwa Urusi ni nchi pekee duniani ambayo watu wake wanatumia muda mwingi sana mitandaoni kuliko nchi yoyote duniani ikiwa na wastani wa saa 6.6 kwa mwezi ukilinganisha na wastani wa kawaida wa dunia nzima ambao ni saa 3.7! Kwa hiyo kuna jamii kubwa sana ambayo inatumia mitandao ya kijamii kwa shughuli mbali mbali. Jamii forum kwa mfano ni mtandao ambao umekuwa ukikutanisha watanzania wengi sana katika masuala ya kijamii. Mtandao huu una idadi ya wanachama 80,867 (Takwimu za Juni 25, 2012) waliosajiriwa na mamilioni ya watu ambao hawajasaliri lakini wanautembelea mtandao huu kila siku. Kama kuna jambo lolote Tanzania limetokea kimbilia Jamii forum utaona mambo yake. Kwa hiyo mitandao hii ya kijamii kuna jamii kubwa sana imo huu mitandao ikikutana pamoja kwa ajiri ya mambo mbali mbali ya kijamii. Toleo lijalo nitaongea kwa upana na marefu kuhusu faida na hasara na kukamilisha makala hii ya athari za mitandao ya kijamii katika maisha ya watu.
Hii ndiyo Teknolojia Yetu.

No comments:

Post a Comment