WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Monday, April 28, 2014

MSHTUKO WA MOYO NI NINI?

Mshituko wa moyo unatokea wakati mtiririko wa damu yenye oksijeni unapozuiwa kwa ghafla katika misuli ya moyo. Iwapo mzunguko huo wa damu hautoendelea haraka, kitendo hicho huifanya misuli ya moyo kuharibika kwa kukosa oksijeni na hivyo kuhatarisha maisha ya muathirika. Mshituko wa moyo kwa lugha ya tiba unajulikana kama 'Myocardial Infarction' inayomaanisha "Myo".. muscles au msuli, 'cardio'.... Heart au moyo na "infarct"....kufa kwa tishu kutokana na kukosa oksijeni. Kama vilivyo viungo vingine mwilini hasa misuli, moyo nao huhitajia damu. Bila damu seli za moyo hudhoofika suala ambalo hupelekea mtu kuhisi maumivu. Mshituko wa moyo hutokea pale mshipa mmoja wa damu au zaidi inaposhindwa kusafirisha damu yenye oksijeni katika moyo, kutokana na kuziba mishipa hiyo. Mishipa ya damu inaweza kuziba kwa sababu tofauti kama vile, kuta za mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo (coronary arteries) kuwa nene, chembechembe za mafuta kujikusanya katika mishipa ya damu, kudhoofika na kukonda mishipa ya damu, mishipa ya damu inaposinjaa na kushikana au spasm na kujitokeza donge la damu katika mishipa ya damu.



                                                          
Mshituko wa moyo mara nyingi husababishwa na ugonjwa wa moyo wa mishipa ya damu au Coronary Heart Disease (CHD). Hii ni hali ambayo ndani ya mishipa ya damu hutokea kitu kiitwacho 'plaque' na kuzuia damu isiweze kupita katika mishipa ya damu, ambayo ni matokeo ya muda mrefu. Lakini ni wakati gani mtu hukabiliwa na hatari ya kupata mshituko wa moyo? Ni pale umri wa mtu unapoongezeka na kuwa mzee, mtu anapokuwa na unene wa kupindukia, kuvuta sigara,  kuwa na shinikizo la damu au High Blood Pressure. Kuishi bila kuwa na harakati na kutoushughulisha mwili. Mtu kuwa na kiwango cha juu cha mafuta katika damu au High Blood Cholesterol. Kuwa na ugonjwa wa kisukari na kuwa na msongo wa mawazo, wasiwasi na fikra nyingi. Mambo mengine yanayochangia kupata mshituko wa moyo ni baadhi ya magonjwa ya moyo, kufanyiwa operesheni ya moyo, kuwa na ndugu katika familia ambao wana matatizo ya moyo na jinsia ya kiume. Tunaelezwa kuwa, uvutaji sigara husababisha mshituko wa moyo unaotokana na kuziba mishipa ya damu kwa asilimia 36, ambapo unene husababisha ugonjwa huo kwa asilimia 20. Kukaa bila kujishughulisha au kufanya mazoezi husababisha mshituko wa moyo kwa asilimia 7-12. Pia wanaume wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo zaidi kuliko wanawake katika kipindi chote cha maisha hasa kabla ya wanawake hawajafikia wakati wa kukatika hedhi. Lakini kwa ujumla kwa kuwa wanawake huishi miaka mingi kuliko wanaume, magonjwa mengine ya moyo husababisha vifo vya wanawake uzeeni zaidi kuliko wanaume.

Saturday, April 12, 2014

TANGAZO KUHUSU MATOKEO YA USAILI KADA YA MIFUGO, UVUVI NA KILIMO MARCH 2014

Wasailiwa waliofanya usaili kuanzia tarehe 4 hadi 15  Machi, 2014 kwa kada za  Kilimo, Mifugo na Uvuvi wametakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa watakaokuwa wamefaulu usaili huo kuanzia tarehe 28 Aprili, 2014.
Naibu Katibu wa Idara ya Ajira katika Sekretarieti ya Ajira Bw. Lucas Mrumapili amesema hayo leo wakati akiongea na baadhi ya wasailiwa waliomtembelea ofisini kwake ili  kujua matokeo ya usaili wa kada za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Sasa hivi kuwapa matokeo yenu hapa siwezi maana kuna taratibu zake ila ninachoweza kuwaeleza ni kwamba mchakato mzima wa usaili huo uko katika hatua za mwisho ambapo hivi sasa tunaandika barua za kuwapangia vituo vya kazi wale waliofaulu usaili kulingana mahitaji ya Waajiri. Hivyo ni vyema nyote mkatembelea tovuti yetu mwishoni mwa mwezi huu tutakuwa tumeshatoa matokeo” alisema Mrumapili.

Alifafanua kuwa ambao hawataona majina yao pindi tangazo litakapowekwa hewani watambue kuwa hawakufaulu usaili husika kwa kiwango kinachotakiwa, hivyo pindi watakapoona matangazo mengine ambayo wanasifa zinazotakiwa wasisite kuwasilisha maombi yao kwa mara nyingine.
Wakati huo huo, Mrumapili amewataka waombaji wa tangazo la kazi la tarehe 22 Januari, 2014 ambalo mwisho wa kupokea maombi ilikuwa tarehe 5 Februari, 2014 kuwa usaili wake umeshaanza kwa baadhi ya kada na kwa kada zilizobakia mchakato wa kuwaita waombaji wenye sifa  kwa ajili ya usaili unaendela.
Pia amefafanua kuwa kwa waombaji wa tangazo la tarehe 17 Februari, 2014 ambalo mwisho wa kupokea maombi ilikuwa tarehe 3 Machi, 2014 mchakato wake nao uko katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuitwa kwenye usaili.

Naibu Katibu  amesema kuwa ofisi yake imefunga kupokea maombi ya kazi kwa  tangazo  la tarehe 18 Machi, 2014  kwa kuwa mwisho wa kupokea maombi  hayo ilikuwa tarehe 3 Aprili, 2014. Aliongeza kuwa kwa tangazo la tarehe 1 Aprili, 2014 ofisi yake bado inaendelea kupokea maombi ya kazi kwa tangazo husika hadi tarehe 15 Aprili, 2014.
Mwisho amewataka waombaji wote wa fursa za ajira Serikalini pindi wanapotuma maombi yao kuzingatia masharti na maelekezo yaliyotolewa katika tangazo husika ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuitwa kwenye usaili.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz  na Facebook-page ya “Sekretarieti Ajira”
au simu 255-687624975
 11 Aprili, 2014.

Wednesday, April 9, 2014

UJUZI NI MUHIMU SANA

  Watu wengi hubaki na maswali kichwani yasio kua na majibu ila si kweli kwamba hayana majibu ila ni nguvu na ari ya kujituma na kuto kata tamaa. kama kweli hakuna majibu basi ni swala la kushirikisha mawazo ya vichwa mbalimbali na kupata majibu ya uhakika. siamini kwamba tumezaliwa masikini na hatuwezi kujikwamua kwenye gurudumu hili,




  lahasha, ninacho amini tunaweza kufanya mapinduzi na tukawa kama hao wanao jiita matajiri.

  Sidhani kwamba watu hupenda kua masikini au fukara ila swali hubaki ni njia gani ambayo tunaweza kufanya ili tuondokane na hii adha. hapo ndipo hutokea watu kuiba, kuuza madawa na kufanya biashara ambazo wanahisi zinaweza kuwaongezea kipato na kuwa matajiri ghafla ingawa biashara zenyewe si halali lakini hujitoa muhanga na kufanya.

   Pamoja na hayo wengi hasa vijana hatuna subira kabisa katika hili ila nataka tu kutoa ushauri kupitia makala hii kwamba tambua wewe kama kijana unaishi na watu tofauti na wana uelewa tofauti. Na maisha safari ingawa hatujui ni safari fupi au ndefu, Lakini utajiri hutoka kwa mungu kuptia watu, watu hawa wana ujuzi tofauti, ujuzi huu uwe wa halali na tujitahidi kuujua ujuzi huu ili tuweze kufika sehemu nzuri. haijalishi tutachukua muda gani kujua ujuzi huu ila tunamafanikio gani katika ujuzi huo na mafanikio sio kupata pesa tu lahasha ila ni umepiga hatua gani au umejifunza nini kupitia ujuzi huo.

Hili ni la muhimu sana pasi na unavyo fikiri kijana wa sasa. Sasa swali linabaki kwako utafanya ujuzi gani na kwa nani ili tuwe kama wale walo weza katika hili..

Sunday, April 6, 2014

AJIRA MIFUGO NA KILIMO

Ni secta ambayo huonyesha kusuasua sana katika kuajiri wasomi ambao wapo wanaranda mtaan mpaka sasa sijajua tatizo ni nini hasa kiasi cha kukaa muda mrefu sana ndipo waajiri. hii ni kwa mtazamo wangu ni kwamba secta ya elimu imeonyesha kujali sana walimu wanao maliza chuo na kutoa ajira kwa asilimia 90.

lakini haipo ivyo katika wizara ya kilimo na mifugo pia katika wizara ya maliasili na utalii. si kwamba wizara hizi naziponda au kushusha hadhi yake lakini ni waizara ambazo hutoa ajira kidogo sana asilimia moja kati ya mia ndio huajiriwa kulingana na wahitimu waliopo mitaani. Waende wapi kama wizara ya mifugo haijaajiri watu wa kutosha miaka mitatu sasa imepita. Haijatosha wamefanya interview mwaka huu lakini bado kimya. Kimya kinamaansha nini?
                                           


    
   Hili ni swali ambalo linatakiwa lijibiwe na wizara ya kilimo na mifugo pamoja na wizara ya maliasili na utalii basi kama ajira hazipo wajulishwe kuliko kubanana huku mtaani na kushindwa cha kufanya. Ingawa kujiajiri ni kuzuri lakini kwa staili hii ya kuwajaza watu mtaani na kuwapa moyo watapewa ajira alafu hakuna chochote kinachoendelea si uungwana
  Hichi ni kilio cha wanakilimo na wanamifugo wapewe fursa na sio kuwaacha njia panda. Huu ni mtazamo tu

TAMAA NI BALAA

  Mara nyingi watu huendeshwa na moyo pia fikra, unapoendeshwa na moyo mara nyingi huwa ni tamaa ila mara chache huwa ni kweli. pia fikra nazo zina pande mbili vile vile tamaa na kweli.

  Sasa nini maana ya tamaa, Ni kile kitu ambacho unapenda kiwe pasi na kushirikisha vitu viwili yani moyo na fikra. hii ni maana fupi tu ya neno tamaa. kwa maana hiyo tamaa huwa inakuja kwa kushirkisha kitu kimoja tu yani moyo au fikra.

  NINI ATHARI ZA TAMAA
Mara nyingi tamaa huja pale ambapo huna kitu lakini unatamani kuwa nacho. hutokea kwa tajiri au masikini. Mara nying hasa vijana huwa na tamaa mbalimbali kama za kimwili au tamaa ya pesa. tunapenda kuwa na wanawake wazuri pia tunapenda kuwa na nyumba, magari ya kifahari na kuwa mastar kabla ya muda hujafika na vitu hivi tunapenda vije haraka sana na hilo ndio kosa letu. Hii hufanya watu kuuwa wenzao na pia kuwekeana vilema na kuwa watu makatili zaidi ya wanyama. Imani yetu ipo wapi kama binadamu tunakuwa zaidi ya wanyama. yote hii kwa sababu ya pesa na mapenzii na hapa ndipo tamaa huitwa balaa kila siku vioja na skendo zisizo kwisha.na mwisho wa tamaa ni majuto na aibu.



USHAURI
Tamaa tuache vijana wenzangu lazima tushirikishe moyo, fikra na akili ndipo tuchukue maamuzi sahihi katika maisha tamaa ndio huponza kichwa na mwili. Tambua tamaa ni balaa..

Wednesday, April 2, 2014

FIKIRI FIKRA YAKO KABLA YA KUKIRI

  ni moja ya msamiati ambao watu wengi hufanya kabla ya kufikiri na hivyo hujutia baadae baada ya kukiri. hii inamaanisha vitu vingi ambavyo kama kijana au mtu mzima ambae una uhuru wa kufanya lolote katika taifa hili una akili timamu ambayo unaweza kuitumia kufanya vitu vinavyo leta maana katika jamii.
                                        
                                                 
   unapo fanya vitu ambavyo vinafurahsha jamii na wewe pia unakua katika wakati mzuri wa kukubalika na jamii na kufanya mambo yako yote yaende sawa kama vile watu kukuamini katika mambo yako na kukupa dhamana ya kufanya vitu vingi zaidi.

                                        
  katika jamii ya sasa ukiwa na fikra nzuri katika kufanya jambo fulani ni hatua nzuri katika maendeleo yako hii inawahusu sana vijana rika yangu.
                                         
                                        


  kabla hujakiri kukosea fikra yako fikiri tena na tena ili kufanya vyema katika mambo yako. Hii ni ushauri tu,