WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Tuesday, November 27, 2012

NINI KILINITOKEA MASAA KABLA YA KIFO CHA SHAROMILIONEA

sharomilionea enzi ya uhai wake
Ni wazi kuwa tanzania nzima kwa ujumla tumeguswa sana na kifo cha msanii wa kuchekesha sharo milionea. lakini kwa upande wangu nimeguswa zaidi kwa kuondoka kijana huyu mdogo ambae alikua akijitengenezea maisha yake ili aweze kujiweza kipindi cha uzee wake ama kweli kifo ni sekunde. hakijapita kipindi kirefu msanii wa kuigiza steven kanumba kuaga dunia na watu kupata mshtuko sana na kifon chake, na uhuhuda ukaonekana kwa kanumba kwamba alijua kwmba anakufa kulingana na matukio ya siku ile alio fariki, vivyohivyo kwa sharomilionea pindi anachati katika twte masage yake ya mwisho ilikua hivi...




gari alilopatia ajali baada ya ajali
siku hii ya tarehe 26 sitaisahau kwni pindi kabla sjapata taarifa ya msiba wa sharomilionea nilishuhudia ajali kubw mbaya sana iliyotokea maeneo ya tengeru wilaya ya arumeru arusha mtu kagongwa na gari aina ya fuso na kukanyagwa mwili mzima na kutolewa ubongo wote nje, baada ya hapo mida ya saa mbili usiku napigiwa simu na mwanahabari mwenzangu alioko tanga katika kituo cha habari mwambao akiniambia sharo milionea apata ajali maeneo ya muheza. nilihisi ni ndoto. lakini ilinibidi niamini kwani kazi ya mungu haina makosa mungu ailaze mahali peema peponi roho ya sharo mahali pema peponi amiin.

mwili wa sharomilionea baada ya ajali






Friday, November 16, 2012

MAAJABU YA TANZANIA









pamoja na amani ya nchi yetu tumejaaliwa kuwa na mbuga, mito, uoto mzuri tamaduni zenye kuvutia na wanawake wenye muonekano mzuri ni fahari yetu Tanzania. naipenda tanzania wewe je, i welcome all people in Tanzania and i respect Tanzania. HAYA NDIO MAAJABU YETU

Wednesday, November 14, 2012

MAMBO MATANO [5] YALETAYO UWEZO WA FIKRA

kwa salamu niseme asalam aleykum kwa wale waislam na bwana asifiwe kwa wale wakristo bila kusahau wale vijana wenzangu mambo vipi. napenda kuwakaribisha katika blog yangu mpya kabisa ambayo imesheheni habari motomoto. kwa vijana na rika zote kwa ujumla.

kama kijana wa kisasa umekabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha kulingana na mfumo mzima wa maisha ya sasa yalivyo badilika. vijana wengi wa sasa wanashindwa kupambanua mambo na kujikuta katika hali ngumu ya kimaisha na kushindwa kujimudu kimawazo na hatimaye kupoteza dira ya maisha. nataka kukueleza ewe kijana wa sasa mambo matano ambayo yatafanya uweze kufikiria kwa kina mambo ambayo unaweza kukutana nayo katika maisha. nayo ni kama ifuatavyo

1. kuwa sambamba na muda, hakikisha katika maisha unakuwa sambamba na muda hii inakusaidia kufanya mambo kwa wakati na inaleta muhemko katika akili kwamba kwa muda huu ninatakiwa nifanye nini

2. pendelea kusoma vitabu au magazeti pindi unapokua uko free na kazi zingine, hii inafanya akili kupevuka kwa haraka na kujua vitu vingi.

3. michezo kama mpira, drafti, basket ball na mingine huitaji akili kuicheza na pia hutuliza akili kwa kujifurahisha, hufanya akili kua active.

4.fanya kazi muda mwingi kuliko kukaa katika vijiwe na kupiga soga, kukaa kwenye vijiwe kwa vijana kuna dumaza akili kwa sababu vijiwe huleta maneno machafu namaranyingine kugombana pasipo sababu ya msingi.


5. kula vyakula vya protini na wanga hivi huleta mabadiliko katika akili na kukufanya uwe na fikra nzuri pindi unapofanya mambo ya busara