kwa salamu niseme asalam aleykum kwa wale waislam na bwana asifiwe kwa wale wakristo bila kusahau wale vijana wenzangu mambo vipi. napenda kuwakaribisha katika blog yangu mpya kabisa ambayo imesheheni habari motomoto. kwa vijana na rika zote kwa ujumla.
kama kijana wa kisasa umekabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha kulingana na mfumo mzima wa maisha ya sasa yalivyo badilika. vijana wengi wa sasa wanashindwa kupambanua mambo na kujikuta katika hali ngumu ya kimaisha na kushindwa kujimudu kimawazo na hatimaye kupoteza dira ya maisha. nataka kukueleza ewe kijana wa sasa mambo matano ambayo yatafanya uweze kufikiria kwa kina mambo ambayo unaweza kukutana nayo katika maisha. nayo ni kama ifuatavyo
1. kuwa sambamba na muda, hakikisha katika maisha unakuwa sambamba na muda hii inakusaidia kufanya mambo kwa wakati na inaleta muhemko katika akili kwamba kwa muda huu ninatakiwa nifanye nini
2. pendelea kusoma vitabu au magazeti pindi unapokua uko free na kazi zingine, hii inafanya akili kupevuka kwa haraka na kujua vitu vingi.
3. michezo kama mpira, drafti, basket ball na mingine huitaji akili kuicheza na pia hutuliza akili kwa kujifurahisha, hufanya akili kua active.
4.fanya kazi muda mwingi kuliko kukaa katika vijiwe na kupiga soga, kukaa kwenye vijiwe kwa vijana kuna dumaza akili kwa sababu vijiwe huleta maneno machafu namaranyingine kugombana pasipo sababu ya msingi.
5. kula vyakula vya protini na wanga hivi huleta mabadiliko katika akili na kukufanya uwe na fikra nzuri pindi unapofanya mambo ya busara
No comments:
Post a Comment