WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Friday, January 25, 2013

BAADHI YA MATUKIO YA PICHA KATIKA MAADHIMISHO YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.W.A MKOANI ZANZIBAR


Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Mtafsiri Lugha kwa njia ya alama akitoa tafsiri ya maneno yanayozungumzwa wakati wa Hafla ya sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Wake za Viongozi na Akinamama wakisikiliza Maulid Barzanj ya Kuzaliwa kwa yaliyosomwa na wasomaji mbali mbali na Qasida katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akitiwa Marashi wakati wa kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa kwake katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.
Ustadh Ali Twalib Mohamed,wa Kibanda Hatari Mjini Zanzibar akisoma Maulid Barzanj Mlango wa kwanza katika kusherehekea kwa kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment