Lowasa ameyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na
waumini wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato kabla ya
kuanzisha harambee maalum ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa
kanisa hilo.
Amesema kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa mwaka 2006 unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 12 ya vijana
hawana ajira na wengi wa vijana hao wako mijini, asilimia 15 ya vijana
nchini kati ya milioni 25 za vijana ndio wenye ajira, ilihali asilimia
70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 -34 ni kundi kubwa ambalo ni
tegemezi na halina ajira na hii ni kati ya nguvu kazi ya vijana milioni
mbili na nusu ambao wako mijini na hawana ajira.
Amefafanua kuwa
wakati hali hiyo ikitokea vijana 850,000 ambao wamekuwa wakihitimu elimu
ya
msingi, sekondari na vyuo wakiwa tayari kuingia kwenye soko la ajira
lakini inasikitisha kati ya hao, ni asilimi 5 tu ndio wanaopata ajira
ya kudumu, huku asilimia 35 ikijikita katika kilimo ambacho bado
kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo zile za uhaba wa pembejeo.
Amewataka
watanzania wote kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa inawekwa
mipango madhubuti kulinusuru kundi hilo kubwa la vijana wenye utayari wa
kuingia kwenye ajira.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria
harambee hiyo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na
Mbunge wa zamani Nyamagana Lawrence Masha, Mbunge wa Rolya Lameck Airo,
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Christopher Mwita
Gachuma, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega(CCM) Dk. Raphael Chegeni na
Mbunge wa sasa wa Nyamagana(Chadema) Ezekiah Dibogo Wenje.
Kwa
upande wa uwakilishi wa Serikali uliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana Said Amanzi na baadhi ya wafanyabiashara maarufu wa mikoa ya
kanda ya ziwa na baadhi wazee maarufu.
Katika harambee hiyo ya
kusisimua iliyoongozwa na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowasa aliyetoa
shilingi milioni 10 kama mchango wake, jumla ya shilingi milioni 200
zimepatikana hivyo kuvuka lengo la shilingi milioni 150, kumalizia
Ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato Mwanza.
No comments:
Post a Comment