WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Wednesday, December 12, 2012

KUMBUKUMBU YA TULIO WAPOTEZA 2012 JE UNAWAJUA?

 naomba nianze kwa dua mungu ibariki tanzania mungu ibariki afrika si vibaya tukajibu amen kwa kuwa yeye alie umba mbingu na aridhi anapaswa ashukuliwe kwa yote. ni wazi sasa mwaka wa 2012 tunaumaliza zikiwa zimebaki siku chache ili kuukaribisha mwaka 2013. kwa niaba ya waandishi wa habari wanaojitegemea na wasiojitegemea hatuna budi kuwakumbuka watu maarufu na wasanii wa hapa nchini kwetu tanzania walio tuacha na majonzi makubwa tukiwalilia lakini haikua riziki mungu akawachukua tunawaombea gheri baraka mungu awalaze mahalim pema peponi amin.

Ni masikitiko makubwa sana kwa tanzania kuondokewa na watu maarufu na majembe ambao walikua wakitegemewa na familia zao na taifa kwa ujumla ili waweze kuinua uchumi wa tanzani. kwa sasa nchi ambayo ndio inaanza kupata maendeleo kupotelewa na watu ambao walikua ni chachu ya maendeleo ni pigo kubwa sana.


mr ebo akiwa kwenye jeneza tayari kwa safari ya mwisho
  hajapita miezi mingi Tanzania tuliondokewa na mtu muhimu msanii mkongwe wa muziki aliekua akivutia sana watalii na watu ndani ya nchi aliekua akianza kujijenga na kupanda chati kwa kasi sana kwa staili yake aliokua akiitumia ulale pema mr Ebo. ni msanii aliekua mcheshi na muelewa kwa kila jambo alilokua akiambiwa....

  haijapita miezi kadhaa tena tukaondokewa na nguli wa filamu tanzania charles kanumba. tutakukumbuka sana kanumba kwa filamu zako zilizokua zinauza sana ndani na nje ya nchi.....


steven kanumba akiwa kwenye jeneza tayari kwa safari ya mwisho

Pia hatujakaa muda mrefu patrick mutesa mafisango katutoka kiungo wa simba sports club alie tegemewa na timu pia mashabiki wa simba katika kuinua simba mpaka kileleni tutakukumbuka patrick na tanahitaji na tutahitaji watu kama wewe ni pengo kubwa uliacha tanzania na tanzania simba sports club.....



mafisango enzi ya uhai wake





patrick mafisango akiagwa

si hao tu katika kipindi hiki cha 2012 tumepotelewa na msanii wa filamu ambaye pia yeye alikua akifuata nyayo za aliekua mkongwe wa filamu tanzania steven kanumba. tulipotelewa na john stephan a.k.a big mungu amlaze mahali pema.

john stephan enzi ya uhai wake
haikupita siku njingi pia tukampoteza muigizaji pia muimbaji wa muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la sharo milionea kwa ajali ya gari ilio tokea maeneo ya muheza tanga pia hii ilituumiza sana watanzania.


sharo milionea enzi ya uhai wake
ila yote tisa kumi tumuachie yeye muweza wa yote nikimaanisha mwenyezimungu ndie atatoa hukumu kwa sisi sote. mungu aweke roho za marehemu hawa mahali pema peponi amiin. pia tunaomba mungu atufikishe mwaka mwingine kwa amani na upendo tukiwa na afya nzuri, eeh mungu tusaidie. kwa kumalizia ujumbe wangu ni tukeshe tukiomba maana hatujui saa wala siku.

Monday, December 10, 2012

RAYC amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu.


RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. (picha na Freddy Maro).
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”