WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Monday, December 10, 2012

RAYC amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu.


RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. (picha na Freddy Maro).
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, leo mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum
Ray C amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”

No comments:

Post a Comment