naomba nianze kwa dua mungu ibariki tanzania mungu ibariki afrika si vibaya tukajibu amen kwa kuwa yeye alie umba mbingu na aridhi anapaswa ashukuliwe kwa yote. ni wazi sasa mwaka wa 2012 tunaumaliza zikiwa zimebaki siku chache ili kuukaribisha mwaka 2013. kwa niaba ya waandishi wa habari wanaojitegemea na wasiojitegemea hatuna budi kuwakumbuka watu maarufu na wasanii wa hapa nchini kwetu tanzania walio tuacha na majonzi makubwa tukiwalilia lakini haikua riziki mungu akawachukua tunawaombea gheri baraka mungu awalaze mahalim pema peponi amin.
Ni masikitiko makubwa sana kwa tanzania kuondokewa na watu maarufu na
majembe ambao walikua wakitegemewa na familia zao na taifa kwa ujumla
ili waweze kuinua uchumi wa tanzani. kwa sasa nchi ambayo ndio inaanza
kupata maendeleo kupotelewa na watu ambao walikua ni chachu ya maendeleo
ni pigo kubwa sana.
|
mr ebo akiwa kwenye jeneza tayari kwa safari ya mwisho |
|
hajapita miezi mingi Tanzania tuliondokewa na mtu muhimu msanii
mkongwe wa muziki aliekua akivutia sana watalii na watu ndani ya nchi
aliekua akianza kujijenga na kupanda chati kwa kasi sana kwa staili yake
aliokua akiitumia ulale pema mr Ebo. ni msanii aliekua mcheshi na
muelewa kwa kila jambo alilokua akiambiwa....
haijapita miezi kadhaa tena tukaondokewa na nguli wa filamu tanzania
charles kanumba. tutakukumbuka sana kanumba kwa filamu zako zilizokua
zinauza sana ndani na nje ya nchi.....
|
steven kanumba akiwa kwenye jeneza tayari kwa safari ya mwisho |
|
Pia hatujakaa muda mrefu patrick mutesa mafisango katutoka kiungo wa
simba sports club alie tegemewa na timu pia mashabiki wa simba katika
kuinua simba mpaka kileleni tutakukumbuka patrick na tanahitaji na
tutahitaji watu kama wewe ni pengo kubwa uliacha tanzania na tanzania
simba sports club.....
|
mafisango enzi ya uhai wake |
|
patrick mafisango akiagwa |
si hao tu katika kipindi hiki cha 2012 tumepotelewa na msanii wa filamu ambaye pia yeye alikua akifuata nyayo za aliekua mkongwe wa filamu tanzania steven kanumba. tulipotelewa na john stephan a.k.a big mungu amlaze mahali pema.
|
john stephan enzi ya uhai wake |
haikupita siku njingi pia tukampoteza muigizaji pia muimbaji wa muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la sharo milionea kwa ajali ya gari ilio tokea maeneo ya muheza tanga pia hii ilituumiza sana watanzania.
|
sharo milionea enzi ya uhai wake |
|
ila yote tisa kumi tumuachie yeye muweza wa yote nikimaanisha mwenyezimungu ndie atatoa hukumu kwa sisi sote. mungu aweke roho za marehemu hawa mahali pema peponi amiin. pia tunaomba mungu atufikishe mwaka mwingine kwa amani na upendo tukiwa na afya nzuri, eeh mungu tusaidie. kwa kumalizia ujumbe wangu ni tukeshe tukiomba maana hatujui saa wala siku.
No comments:
Post a Comment