Baada ya kuugua kwa muda mrefu, hatimaye aliyekuwa muigizaji wa
filamu nchini, Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki amefariki dunia jana
alfajiri katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,
Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la
upungufu wa damu,mgongo na kansa ya ngozi
Sajuki alikuwa akitakiwa kurejea tena nchini India kwaajili ya
kuendelea na matibabu ya tatizo lililokuwa likimsumbua ambapo jumla ya
shilingi milioni 28 zilikuwa zikihitajika.
Hivi karibuni ilidaiwa kuwa alikuwa ameshakusanya shilingi milioni
saba tu zilizotokana na michango ya watu na show alizokuwa akizifanya
kukusanya fedha hizo. Show ya mwisho aliifanya jijini Arusha ambako
alianguka kwenye stage.
Kifo hicho cha Sajuki kimepokelewa kwa masikitiko makubwa kutoka kwa
watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa Tanzania waliotumia mitandao ya
kijamii kuelezea masikitiko yao.
Mwasiti Almas
Tunapolala na kuamka tunasema AHSANTE kwa mungu,tunapopoteza pia
tunaowapenda tuseme AHSANTE… alichokileta ALLAH chini ya jua atakichukua
Salama A. Jabir
Mwenyezi Mungu Akusamehe Makosa Yako Ndugu Yetu Juma
Kilowoko..Ucheshi Wako Ntaukumbuka Milele. Pumzika Kwa Amani Rafiki.
#RIPSajuki
Jokate Mwegelo
Nimesikia hii habari sasa. Sad lakini kazi ya Mungu haina makosa
tunazidi kumtumainia yeye na kumshukuru. Upumzike kwa amani sajuki.
Amen!!
Zitto Zuberi Kabwe
Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii
nchini kupata kipato stahili na kazi Yao. Kifo chake kimeniondolea Mtu
niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania
walio kwenye entertainment industry. Sajuki left an indelible mark in my
politics. Pumzika Kwa Amani Juma.
Masanja Mkandamizaji
Duniani si nyumbani kwetu. Ni njia tu.
Hemedy Suleiman
R.I.P SAJUKI……..daaaaaah this is painful!!
No comments:
Post a Comment