naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Mh; Januari Makamba |
Hiyo inatokana na kauli ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba aliyoitoa
jana akisema kwamba wizara yake ilipinga tangu awali mpango huo kabla ya kupitishwa na kuwa sheria na kwamba anaamini itaondolewa. Kauli hiyo ya Makamba imekuja siku moja baada ya chama tawala, CCM, kukaririwa na vyombo vya habari kikiitaka Serikali kuangalia vyanzo vingine vya mapato badala ya tozo hiyo
Alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti
kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano
zinapungua... “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza
gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.
“Nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa,
kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni
kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa
kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo.”
No comments:
Post a Comment