WELCOME

"Experience is not what happens to you; it is what you do with what happens to you." and "When you feel like giving up, remember why you held on for so long in the first place"Instead of giving myself reasons why I can't, I give myself reasons why I can." because always "When one door closes another door opens; but we so often look so long and so regretfully upon the closed door, that we do not see the ones which open for us."by ISI H


Wednesday, April 9, 2014

UJUZI NI MUHIMU SANA

  Watu wengi hubaki na maswali kichwani yasio kua na majibu ila si kweli kwamba hayana majibu ila ni nguvu na ari ya kujituma na kuto kata tamaa. kama kweli hakuna majibu basi ni swala la kushirikisha mawazo ya vichwa mbalimbali na kupata majibu ya uhakika. siamini kwamba tumezaliwa masikini na hatuwezi kujikwamua kwenye gurudumu hili,




  lahasha, ninacho amini tunaweza kufanya mapinduzi na tukawa kama hao wanao jiita matajiri.

  Sidhani kwamba watu hupenda kua masikini au fukara ila swali hubaki ni njia gani ambayo tunaweza kufanya ili tuondokane na hii adha. hapo ndipo hutokea watu kuiba, kuuza madawa na kufanya biashara ambazo wanahisi zinaweza kuwaongezea kipato na kuwa matajiri ghafla ingawa biashara zenyewe si halali lakini hujitoa muhanga na kufanya.

   Pamoja na hayo wengi hasa vijana hatuna subira kabisa katika hili ila nataka tu kutoa ushauri kupitia makala hii kwamba tambua wewe kama kijana unaishi na watu tofauti na wana uelewa tofauti. Na maisha safari ingawa hatujui ni safari fupi au ndefu, Lakini utajiri hutoka kwa mungu kuptia watu, watu hawa wana ujuzi tofauti, ujuzi huu uwe wa halali na tujitahidi kuujua ujuzi huu ili tuweze kufika sehemu nzuri. haijalishi tutachukua muda gani kujua ujuzi huu ila tunamafanikio gani katika ujuzi huo na mafanikio sio kupata pesa tu lahasha ila ni umepiga hatua gani au umejifunza nini kupitia ujuzi huo.

Hili ni la muhimu sana pasi na unavyo fikiri kijana wa sasa. Sasa swali linabaki kwako utafanya ujuzi gani na kwa nani ili tuwe kama wale walo weza katika hili..

No comments:

Post a Comment