Ni secta ambayo huonyesha kusuasua sana katika kuajiri wasomi ambao wapo wanaranda mtaan mpaka sasa sijajua tatizo ni nini hasa kiasi cha kukaa muda mrefu sana ndipo waajiri. hii ni kwa mtazamo wangu ni kwamba secta ya elimu imeonyesha kujali sana walimu wanao maliza chuo na kutoa ajira kwa asilimia 90.
lakini haipo ivyo katika wizara ya kilimo na mifugo pia katika wizara ya maliasili na utalii. si kwamba wizara hizi naziponda au kushusha hadhi yake lakini ni waizara ambazo hutoa ajira kidogo sana asilimia moja kati ya mia ndio huajiriwa kulingana na wahitimu waliopo mitaani. Waende wapi kama wizara ya mifugo haijaajiri watu wa kutosha miaka mitatu sasa imepita. Haijatosha wamefanya interview mwaka huu lakini bado kimya. Kimya kinamaansha nini?
Hili ni swali ambalo linatakiwa lijibiwe na wizara ya kilimo na mifugo pamoja na wizara ya maliasili na utalii basi kama ajira hazipo wajulishwe kuliko kubanana huku mtaani na kushindwa cha kufanya. Ingawa kujiajiri ni kuzuri lakini kwa staili hii ya kuwajaza watu mtaani na kuwapa moyo watapewa ajira alafu hakuna chochote kinachoendelea si uungwana
Hichi ni kilio cha wanakilimo na wanamifugo wapewe fursa na sio kuwaacha njia panda. Huu ni mtazamo tu
No comments:
Post a Comment