HATIMAYE
kitendawili cha nani atanyakua taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 kimeteguliwa
usiku huu na mrembo Happiness Watimanywa kutoka Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati
kufanikiwa kutawazwa Mshindi wa taji hilo na kuwashinda warembo wengine 29
waiokuwa wakiwania taji hilo.
Nyota ya
Happiness ilionekana dhahiri kung’aa vyema katika fainali hizo mwaka huu tangu
pale alipofanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa mrembo
wa kwanza kuingia nusu fainali.
Wakati
Happiness akinyakua Taji hilo pamoja na zawadi ya Gari na kitita cha shilingi
Milioni 8 nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo Latifa Mohamed kutoka Kitongoji
cha Kigamboni na Kanda ya Temeke na nafasi ya Tatu ikienda kwa Miss Tanzania
Sports Woman, Clara Bayo.
Pamoja nao
warembo wengine walio ingia hatua hiyo ya tano bora ni Lucy Tomeka na Elizabeth
Prety.
sherehe zikiendelea
burudani ni kawaida
kujichana misosi mizuri zuri
huyu ndie miss tanzania 2013 Happiness Watimanywa akipunga mkono
hili ndilo gari alilo kabidhiwa miss tanzania wengine huita ndinga wengine husema mkoko basi mbwembwe tu.
No comments:
Post a Comment