Ni kazi sana kujua lakini si kazi kuhisi, ni wazi kabisa kua tanzania na dunia kwa ujumla imechafuka kwa kukosa maadili na kufanya mambo ambayo si heshima na si ustaarabu. na je ni nani muhusika mkubwa ambae anachochea tanzania yetu kuharibika na kukosa heshima kwa vizazi vijavyo?
Ni wazi kua kuna pande mbili ambazo zikifanya vibaya yani kukosa heshima na busara basi vizazi vijavyo navyo hukosa heshima na busara.
1. WASANII hawa tunawaita kioo cha jamii pia wanamchango mkubwa sana katika kuipeleka tanzania mbele kuitangaza na kujulikana zaidi. wasanii ni watu ambao wako tofauti hata kimuonekano kwenye jamii. watu wengi hupenda kuwaiga na hupenda kuwa kama wao hasa vijana. lakini pindi msanii akiwa na skendo za ajabu na kujidhalilisha basi na vijana na kizazi kijacho atafanya mambo hayo pasi na kujali na huona ni kawaida.
2.WANASIASA. hawa pia ni watu muhimu ambao huendesha nchi kwa kufuata sheria ya nchi na katiba pindi mwanasiasa akivunja sheria na kutochukuliwa hatua basi wananchi hasa wa hali ya chini huwa hawana amani na kupoteza uaminifu na vurugu.
Kama hivi vitu vitatumika ipasavyo basi tanzania yenye amani na maadili itapatikana na kujenga picha nzuri ndani na nje ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment